Habari za Punde

*TASWA FC KUSHIRIKI BONANZA MAALUM LA MAADHIMISHO YA UHURU WA MIAKA 51 YA TANZANIA


Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, (Taswa FC) ni miongoni mwa timu nane zitakazoshiriki katika bonanza maalum la kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania (Uhuru Dar Corporate Bonanza) lililopangwa kufanyika Desemba 9 kwenye uwanja wa Gymkana.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamepokea mwaliko kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vannedrick (T) Limited, Fredrick Mwakalebela kuhusiana na ushiriki wa timu katika bonanza hilo na wao wamethibitisha.
Majuto alisema kuwa kampuni ya Vannedrick (T) Limited ndiyo imeandaa bonanza hilo na kudhaminiwa na benki ya NMB na wachezaji wake kwa sasa wapo katika maandalizi  ya kina ili kutwaa ubingwa. Bonanza hilo litaanza saa 2.00 asubuhi.
Alisema kuwa timu nyingine ambazo zitashiriki katika bonanza hilo ni Barrick, NMB, Dstv na Radio Times ambazo zipo katika kundi A na Taswa FC pamoja na Jubilee, Azam Group na wenyeji, Gymkhana wapo katika kundi B.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Vannedrick (T) Limited, Mwakalebela alisema kuwa timu hizo zitachuano kwa mtindo wa Ligi na timu mbili katika kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali na baadaye fainali.
Alisema kuwa pia kutakuwa na zawadi za mshindi wa tatu mbali ya mshindi wa kwanza na wa pili. |”Lengo ni kuwaweka pamoja wadau wa michezo ambapo mbali ya kuadhimisha miaka 51, tutatumia fursa hiyo kujadilia masuala mbaali mbali ya michezo, matatizo, mafanikio na nini kifanyike,” alisema Mwakalebela.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.