Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa
Wanawake Tanzania (TWFA) unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini
Morogoro.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA,
Ombeni Zavala, uchaguzi huo utatanguliwa na Mkutano Mkuu wa TWFA. Wajumbe wapiga
kura wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao
ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla (Desemba 18 mwaka
huu).
Wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi ni kama ifuatavyo; wanaowania uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na
Lina Kessy. Rose Kissiwa ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu
Mwenyekiti.
Wanaowania ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia
Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) inagombewa na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa kutokana
na sababu za kifamilia.
Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya
ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila
wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya
28(2).
No comments:
Post a Comment