Habari za Punde

*UZINDUZI WA KAMPENI YA LISHE BORA KWA MAMA NA MTOTO MKOANI LINDI

 Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu (kulia) akikabidhi unga wa lishe na maziwa kwa mkazi wa Lindi, Zainabu Ali na mtoto wake Bright Abdallah, ambaye aliweza kuelezea vizuri masuala ya lishe, katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika
Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
 Mkazi Lindi, Habiba Rashidi, akihamasisha wakazi wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa lishe bora wakati wa maandamano ya watoto, katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
 Baadhi ya watoto wa Lindi wakitembea kwa maandamano katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
 Mkurugenzi wa Shirika la Watoto la Save the Children Tanzania, Rachel Pounds, akizungumza  katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Hamidi Nassoro, Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mafuru Mng’ong’o na Mbunge wa Serengeti, Dk Kwebe Stephen Kwebe.
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mafuru Mng’ong’o, akizungumza katika hafla hiyo.
 Mwanamuziki mkongwe nchini, Kassim Mapili, akifanya vitu vyake pamoja na wasanii wa Mjomba Band, katika hafla ya katikasherehe za uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.
Msanii wa Mashairi, Mrosho Mpoto, akikonga nyoyo za wakazi wa Lindi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.