WAKAZI wa Kijiji
cha Gare, Kata ya Magoroto, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wanaomba wadau na
wananchi wenye mapenzi mema kuchangia ujenzi wa barabara ya Kijiji cha
Kwematindi hadi Gare, kwa kuwa inachangia kuzorotesha uchumi wao.
Mkakati wa kuomba msaada wa ujezni wa barabara hiyo umeanza baada ya kuona Serikali ya Kijiji na Kata hawana mpango wa kuendeleza kijiji hicho ambacho hakina barabara tangu uhuru.
Barabara hiyo imekuwa kikwazo cha shughuli nyingi za kiuchumi, hasa kipindi cha masika, hali inayohitaji jitihada za haraka kuijenga kwa maslahi ya wananchi wa kijiji hicho na Taifa kwa ujumla.
Lakini kutokuwepo kwa barabara hiyo imekuwa ni chanzo cha umasikini kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wengi wao ni wakulima na wanashindwa kufanya shughuli zao za kuinua uchumi kutokana na miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikiwakwamisha kusafirisha bidhaa zao na wananchi kushindwa kufika kijijini kwa urahisi.

Kukosekana kwa barabara hiyo kumewanyima
wanakijiji fursa ya kupata huduma za jamii kama vile shule na hospitali hali
inayochangia kurudi nyuma kimaendeleo.
Barabara hiyo korofi na isiyopitika kwa magari wala pikipiki, inahitaji kuchongwa kwa gharama ya Sh Mil 13,120,000 hali ambayo imekuwa ngumu kwa kuwa wanakijiji wengi hawana uwezo huo kutokana na kukosa kipato na hivyo ni muda muafaka kwa wananchi, hasa wanaoishi Dar es Salam watokao mkoani Tanga, kusaidia harakati za ujenzi wa barabara hii, kwa kuwa baada ya mambo yote nyumbani ni muhimu.
“Naomba niwakumbushe ndugu zangu wanaoishi Dar es Salaam na mikoa mingine na wale wanaoishi nje ya nchi watokao mkoani Tanga wakumbuke nyumbani kwa kuchangia maendeleo kwa kuwa nyumbani ni nyumbani”
Kwa yeyote atakayeguswa achangie kupitia akaunti namba 41910000967 NMB au Tigo Pesa, 0719 242943, M-pesa 0767 216006 na Airtel Money 0786 645765, msaada unaweza kuanzia unapoweza kujikuna.

Imetolewa na Katibu WKGM, Andrew Kibuyu 0767216006
No comments:
Post a Comment