Hoteli ya Double Tree, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, iliyofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) kutokana na kushindwa kudhibiti maji machafu yanayotiririka kutoka katika Hoteli hiyo na kumwagika Baharini bila kujali uchafuzi wa mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira) Dkt. Terezya Hivisa (katikati) akikagua mfumo wa maji taka katika Hoteli ya Double Tree, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kufanya ukaguzi wa mfumo wa maji taka katika hoteli hiyo.
''Haiwezekani, kwa hali hii tunawafungia ili mjifunze'', Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira) Dkt. Terezya Hivisa (katikati) akizungumza na Mkurugenzo Mkazi wa Hoteli hiyo, Karim Kanji (kulia) na kumpa amri ya kuifunga hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment