Safari kubwa ya mwishoni mwa mwaka
ambayo inawakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Tanzania na nje
ya Tanzania kwa ajili ya kwenda kusheherekea kwa pamoja sherehe za mwaka mpya
inatarajiwa kufanyika tena mwaka huu kwa jumla ya siku nne mfululizo visiwani
Zanzibar kuanzia Desemba 31, 2012 mpaka Januari 3, 2013 ikiwa na lengo la
kuwaleta vijana pamoja na kutangaza utalii wa ndani hapa nchini
kwa.
Safari hiyo ambayo imekuwa na
mafanikio tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010/2011 na vijana watatu wa Kitanzania
waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Vijana walio katika Elimu ya juu
inatarajiwa kushirikisha vijana takribani 100 kutoka pande zote za Dunia na
Tanzania kwa ujumla katika kusheherekea kwa pamoja visiwani
Zanzibar.
“Zanzibar Reloaded tumekuwa tukifanya
hivi kila mwaka kwa kutoa nafasi kwa vijana wa Kitanzania na nje ya nchi kuweza
kujumuika pamoja na kusheherekea kwa pamoja katika kaudhimisha ujuo wa mwaka
mpya ikiwa na pamoja na kutafakari changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana
na nini mipango ya kila kijana katika kukabiliana na changamoto hizo” Alisema
Ndg. Gwamaka Mwibuka, Mkuu wa Maandalizi wa Zanzibar
Reloaded.
Safari hii haibagui mtu yeyote kutoka
upande wowote ule wa Dunia kuweza kujumuika pamoja na vijana wenzake kushiriki
katika sherehe hizi, kwani nia ni kutengeneza Muunganiko mmoja wa vijana toka
pande zote za Dunia.
“Hii si safari ya baadhi ya kikundi
cha vijana bali ni safari ya kila kijana ambae anapenda kwenda kufurahia sherehe
za mwaka mpya katika visiwa vya marashi ya karafuu huku akitembelea sehemu
muhimu za utalii visiwani humo, ukiangalia viwango vilivyowekwa vinaendana na
huduma itakayotolewa kwa siku zote nne tangu siku ya kwanza mpaka ya mwisho”.
Aliongeza Gwamaka
Akitaja viwango vya mchango wa Safari
hiyo kwa mtu mmoja ni Shilingi 150,000/= kwa Mtanzania na Dola 160 kwa mgeni
anae nje ya nchi na kufafanua kwamba pesa hizo zitatumika kwa Usafiri wa Boti
Dar-Zanz kwenda na kurudi, Malazi siku zote nne, Chai, usafiri wa kutembea
sehemu mbalimbali, Parties na kiingilio cha Clubs kwa watakaopenda kwenda lakini
akafafanua zaidi na kusema kwamba mshiriki atajihudumia chakula cha mchana na
usiku kwa siku zote hii ni kutoa fursa ya mtu kula kile anachokipenda ikiwa na
kunywa anachokipenda.
“Mwaka huu tumejipanga kuacha
kumbukumbu ya daima ndani ya vichwa vya watakaoshiriki, tutakwenda kutembelea
Prison Island, Dolphin Tour nayo itakuwepo, Tutapata muda wa kutembelea Stone
Town na kufanya Shopping, Kuogelea na kucheza kwa pamoja katika fukwe za bahari
visiwani humo”. Alimalizia Gwamaka.
Unaweza kufanya Booking yako sasa
kupitia website: http://zanzibarreloaded.wix.com/2013, Au ukurasa wa Facebook:
https://www.facebook.com/ZanzibarReloaded kwa picha na taarifa
zaidi.
Zanzibar Reloaded ilianza mwaka
2009/2010 ambapo Vijana watatu wa Kitanzania ambao waliungana pamoja na kutafuta
njia nzuri ya kumaliza mwaka mpya kwa vijana wote wa Tanzania na nje ya Tanzania
kwa lengo ya kubadilishina mawazo pamoja.
Zaznibar
Reloaded ni tukio la kila mwishoni mwa mwaka ambalo hufanyika katika visiwa vya
Zanzibar, tukio ambalo lina lengo la Kusheherekea na kuwaleta vijana kutoka
sehemu mbalimbali za Dunia kwa ajili ya Kufurahi pamoja na kutengeneza
muunganiko imara hii ikiwa pamoja na kujionea maajabu yaliyopo visiwani ambayo
yataimarisha na kuhamasisha utalii wa ndani.
No comments:
Post a Comment