Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo
akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Shirika la Taifa la Bima (NIC) Uganda wakati
wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki kwa mchezo wa Netiboli,
ambayo walicheza na JKT – Mbweni ya ya Tanzania juzi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo
akimkabidhi Kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya netiboli Klabu Bingwa
Afrika Mashariki nahodha wa Timu ya NIC Uganda ,Obua Desire, baada ya kuifunga
timu ya JKT Mbweni ya Tanzania magoli 47 – 30 jana jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya NIC Uganda wakifurahia ushindi uliopelekea
kutetea ubingwa wao juzi jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Netiboli Tanzania (Chaneta)
Bi. Anna Kibira 9kusoto) akikabidhiwa majukumu ya Shirikisho la vyama vya mpira
wa netiboli Afrika Mashariki (EANA) na Rais wa Shirikisho hilo Bi.Mildred
Ajiemba Wanyama juzi jijini Dar es Salaam. Tanzania imekabidhiwa kuongoza
sekretariati ya shirikisho hilo kutoka nchi ya Kenya. Picha na Frank
Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM




No comments:
Post a Comment