Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki
akifungua rasmi mafunzo ya stadi za uchunguzi yanayofanyika katika hoteli ya
Naura Spring jijini Arusha.
Mafunzo hayo ya wiki moja yalianza Machi 31—4, 2014 yamelenga kuwaongezea maafisa
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) stadi za kiuchunguzi hasa
wanapofanya uchunguzi unaohusiana na kazi za kila siku za Polisi.
Kushoto ni
muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi. Lindiwe
Khumalo na kulia ni Muwezeshaji Mkuu wa
mafunzo hayo Bwana Sean Tait kutoka African Policing Civilian Oversight Forum
(APCOF).Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la GIZ.
Maafisa Uchunguzi wa THBUB wakijifunza kwa vitendo namna ya
kukabiliana na Matukio yanayohusiana na uvunjwaji wa haki za binadamu.
Sehemu ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto
ni Afisa Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Msaada wa Sheria, Bwana Nabor Assey na anayeonekana kwa mbali ni
Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula
Sehemu ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto
ni Afisa Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Msaada wa Sheria,Kushoto ni Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiwasilisha Mada ya
kwanza inayohusu Haki za binadamu na masuala ya Polisi.
Maafisa wa THBUB wakijadiliana katika kazi za vikundi ambazo ni sehemu ya
Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala Bora, Hajat Fatuma Muya
akichangia jambo katika mafunzo hayo.Anayemsikiliza ni Afisa Uchunguzi, Bi. Farida Ndege.
Maafisa Uchunguzi wa
THBUB wakifanya mafunzo kwa vitendo kutoka ( Kushoto) ni Bi. Vivian Method na (kulia) ni Bi. Makihiyo
Mrutu
Sehemu ya washiriki wakipitia makabrasha wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini
Bibi Lindiwe Khumalo akichangia jambo katika mafunzo hayo, kulia ni Muwezeshaji
Bi. Louise Edwards.
Maafisa
Uchunguzi wa THBUB katika kazi za
vikundi wakati wa mafunzo.
Bwana Mokgapi Maleka , Afisa kutoka shirika la GIZ la Afrika
Kusini ambalo ndio wafadhili wakuu wa Mafunzo hayo akiongea na washiriki.
Muwezeshaji wa Mafunzo kutoka THBUB, Bibi Jamila Sulu
akiwapa maswali ya “chemsha bongo” Maafisa wa THBUB kwa lengo la kupima
kumbukumbu ya kile walichojifunza.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na
wawezeshaji.
Muwezeshaji kutoka African Policing Civilian Oversight Forum
(APCOF) akiwasilisha mada inayohusu
Uandaaji wa ushahidi Mahakamani.
No comments:
Post a Comment