Habari za Punde

*WAJUMBE WAPYA WA ZIADA WA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM WATANGAZWA

Na Magreth Kinabo- Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametangaza rasmi majina  mengine ya ziada ya wajumbe wapya wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo.
Majina hayo yametangazwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge  hilo, Samia Hassan Suluhu  mjini Dodoma kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge hilo.
 Taarifa hiyo ilieleza kwamba Mwenyekiti huyo amefanya uteuzi huo, ili kuleta muafaka  kwa kushirikisha  wadau kutoka uwakilishi wa upinzani, ambao hawakuweza kuchaguliwa kwenye kamati 12 za Bunge  hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo aliyataja majina hayo kuwa ni Freeman Mbowe, Abubakar  Khamis Bakari, Fatma Abdulhabib Fereji, Nakazael  Lukio Tenga na Amon  Mpanju.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.