Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa
(kushoto) akitoa elimu kuhusu ujasiriamali na baadhi ya vijana kutoka
vyuoni walio katika kambi maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Maa
Media kwa udhamini wa NBC mjini Bagamoyo, Pwani hivi karibuni. NBC
ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 ambapo mbali na ujasiriamali
vijana hao walifundishwa pia madhara na jinsi ya kuepuka matumizi ya
madawa ya kulevya.
Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kulia), akisalimiana na
Meneja Miradi wa Kampuni ya Maa Media, Albany James wakati yeye na
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa
(kulia) walipotembelea kambi ya vijana iliyoandaliwa na Maa Media ili
kuwafundisha masuala ya ujasiriamali, madhara na jinsi ya kuepukana na
matumizi ya madawa ya kulevya. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs
milioni 100 kwa ajili ya kambi hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo. Wa pili
kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lekoko Furaha.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Rukia Mtingwa akifanya
mahojiano na waandishi wa habari wakati uongozi wa benki hiyo
ukitembelea kambi ya vijana iliyoaandaliwa na Maa Media kwa udhamini wa
benki ya NBC.
Vijana wakijiweka sawa kabla ya kuanza kwa mafunzo yao.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda (wa pili kulia)
akikabidhi msaada wa vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi
wa kituo cha watoto yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio
kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani mjini Njombe hivi karibuni
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Njombe, Sady Mwang’onda akifanya
mahojiano na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada wa
vyakula, sabuni, mafuta na vitu vingine kwa walezi wa kituo cha watoto
yatima cha Imiliwaha ikiwa ni moja wa matukio kuadhimisha Siku ya Ukimwi
Duniani mjini Njombe.
No comments:
Post a Comment