Habari za Punde

*HADIJA MWANAMBOKA AIBUKA NA VITU VYA HADIJA KINONDONI BLOK 41

 Mwanamitindo mahiri nchini Khadija Mwanamboka, amefungua kiota kipya kabisa maeneo ya Kinondoni Blok 41 kinachotoa huduma ya mambo ya maakuli na vinywaji laini, ikiwa ni pamoja na Juice fresh za matunda mbalimbali kama Embe. Pasion, Nanasi, Fenesi, na mengineyo mchanganyiko, pamoja na vyakula vya aina mbalimbali vinavyopatikana kwa mtindo wa Bufee. Eti ni 'VITU VYA KHADIJA' fika ukajionee mwenyewe Vitu vya Hadija, Kiota hicho kimefunguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Ramani ya kufika kiotani ni, ukitokea barabara kubwa ya Kinondoni maeneo ya Biafra unakata kushoto, kona ya kwanza kushoto kwako tena unanyoola utakutana na kibao hiki, pia unaweza kutokea nyuma ya jengo la Airtel Moroco.
 Mandhari ya ndani ya kiota hicho ni kama hivi meza na viti vyote ni rangi pendwa.....
 Mandhari ya kiotani
Menu ya huduma zinazopatikana mahala hapo.
 Pia ukifika hapo utapata vitu kama hivi ndani ya Supermarket iliyopo kiotani hapo
 Ndani ya Supermarket
 Ufuta...na vinginevyo
Vitu vya Hadija ni utamu haji mwisho....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.