*SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya Alex Bw.Massawe, kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star) na klabu ya Simba SC, Christopher Alex kilichotokea jana mjini Dodoma.
Christopher Alex Massawe aliwahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mwanzoni mwa miaka ya 2000's na kwa mafanikiko makubwa huku pia akiwa tegemeo katika klabu yake ya Simba SC.
Katika salam zake kwa familia ya Massawe, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.
*MWADUI FC BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL)
Timu ya Mwadui kutoka mjini Shinyanga jana imetawazwa kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuifunga timu ya African Sports ya jijini Tanga kwa bao 1 - 0, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Comlex Chamazi jijni Dar es alaam.
Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui ushindi katika mchezo huo wa fainali.
Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni 2.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/205.
Jumla ya timu nne zimepanda Ligi Kuu msimu ujao ambazo ni Bingwa Mwadui FC, African Sports, Majimaji na Toto Africans.

No comments:
Post a Comment