Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akikimbia kushangia bao lake la kwanza alilofunga kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na Andrey Coutihno. Kushoto ni beki wa timu hiyo, Oscar Joshua na (kulia) ni beki pia Juma Abdul. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons huku Msuva akitupia mawili na Coutinho moja kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Coutinho, baada ya kufunga moja kati ya mabao matatu yaliyofungwa na timu hiyo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo jioni kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Amis Tambwe (kushoto) akiambaa na mpira kumpita beki wa Tz Prisons wakati wa mchezo huo.
Coutinho (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Prisons.
Kocha mkuu wa Yanga, akimpongeza Msuva, baada ya kuifungia timu yake katika mchezo huo.





No comments:
Post a Comment