Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam jana tayari kwa kukagua ujenzi wa maabara na pia kupokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea baadhi ya vitabu vya sayansi kutoka kwa Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Vitabu hivyo ambavyo vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakisalimia wanafunzi katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, wakiongea na mkandarasi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress akigawa vitabu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi jijini Dar es salaam. Vitabu hivyo, ambavyo pia
vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakiangalia jinsi somo la sayansi likifundishwa katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani.
No comments:
Post a Comment