Sehemu ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura katika zoezi hilo lililoanzia Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoa wa Njombe jana, ambapo wananchi waliitikia wito kwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha zoezi hilo.
Zoezi hilo litaendelea kwa muda wa siku saba katika Halmashauri hiyo ya mji wa Makambako baada ya kuzinduliwa rasmi leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda .
Hii ni moja kati ya kadi za wapiga kura zilizokamilika jana na kukabidhiwa kwa wenyewe.
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha katika daftari hilo.
Hapa ni wananchi wa Mtaa wa Matema wakiwa kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo katika foleni ya kujiandikisha katika daftari hilo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (wa pili kulia) akizungumza jambo na viongozi wenzake walipofika kutembelea zoezi hilo.
Baadhi ya wanahabari wakiwahoji wananchi wakati wa zoezi hilo.
Wananchi katika foleni ya kujiandikisha.
Wananchi katika foleni ya kujiandikisha huku wengine wakihojiwa na wanahabari.
Hawa wakisubiri utaratibu...
Wakisubiri utaratibu......
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, akihojiwa na wanahabari
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, akihojiwa na wanahabari.













No comments:
Post a Comment