Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akijumuika pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu katika kumsalia Bibi Fatma Moh’d Othman aliyefariki Da es salaam juzi na kuzikwa Kijijini kwao Kiwani Wilaya na Mkoani Pemba.
Balozi Seif pamoja na baadhi ya viongozi wakiwasili makaburini kwa ajili ya Mazishi ya Bibi Fatma Moh’d Othman, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.
Maakamuj wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpa pole Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid ambaye ni Mtoto wa Marehemu Bibi Fatma hapo nyumbani kwake Mtaa wa Mfenesi Mazizi Mkoani.
Balozi Seif akijumuika pamoja na waumini na wananchi katika kuufukia mwili wa Marehemu Bibi Famta Moh’d Othman katika makaburi ya familia yao hapo Kiwani.
***************************************************
Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo amejumuika pamoja na Wananchi amoja na wana wa Familia katikia maazishi ya Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Utumishi Serikalini Bibi Fatma Moh’d Othman aliyezikwa kijijini kwao Jimbo la Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.
Marehemu Bi Fatma Moh’d alifariki Dunia Jana katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Shindikizo la Damu { Blood Pressue }.
Balozi Seif katika mazishi hayo akitanguliwa na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pia aliambatana na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Ali Abdulla Ali, Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Nassor Jazira, Mwakishi wa Jimbo la Kkwahani Mh. Ali Salim Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali vyama vya siasa pamoja na Dini.
Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman ambae ni Mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid katika uhai wake alishika nyafidha mbali mbali za Kiserikali amoja na Kisiasa.
Katika utumishi wa Serikali Marehemu Bi Fatma aliwahi kuwa Mwalimu Mkuu wa Skuli za Ngomeni na Mkoani Pemba, Afisa wa Elimu Wilaya ya Mkoani, Mratibu wa Uendeshaji na Utumishi Elimu Pemba Pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Utumishi Serikalini wadhifa alioutumikia hadi kufikwa na mauti.
Aidha katika utumishi wa Kisiasa Mrehemu Bi Fatma alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanakwake Tanzania { UWT } Wilaya ya Mkoani, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa CCM, Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi pamoja na
UWT.
Pia alikuwa Mjumbe wa Kamati tekelezaji Wilaya ya Mkoani Wazazi na UWT, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mainduzi Mkoa kuanzia mwaka 21 hadi 215 pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman aliyezaliwa mwaka 1950 na kufikia umri wa miaka 65 ameacha Watoto Tisa na Wajukuu kadhaa.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Bibi Fatma Moh’d Othman mahali pema Peponi. Amin.




No comments:
Post a Comment