Mchezaji mpya wa Yanga, Godfrey Mwashiuya (kulia) akimtoka beki wa SC Villa kwa speed kali wakati wa mchezo wa kirafiki wa Hisani uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 0-0.
Mwashiuya, akiendelea kuwatesa mabeki wa SC Villa....
Huyu beki naamini alikoma na aliwasimulia wenzake kwa vyovyote vile....maana kazi aliyopewa na dogo huyo haikuwa ya kitoto.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.
Shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga aliyezoeleka kuonekana akiwa amejipaka 'masinzi' hapa leo akitoka kivingine akiwa amevunja Suti na Tai ya Yanga, ila hii imeelezwa kuwa ni baada ya kuoa hivi majuzi.
Mpiga picha wa Azam Tv Iddi akiwajibika kurusha live uwanjani hapo....
Mashabiki wa Yanga wakimshangilia mchezaji mpya wa Yanga, aliyetua kujiunga na wakali hao, akitokea Zimbabwe, Ngoma, akiwa jukwaani akishuhudia mchezo huo...
Ngoma akitambulishwa kwa mashabiki.

Ngoma akitambulishwa kwa mashabiki.
Deus Kaseke naye aliwatesa mabeki wa Villa, hapa akimfinya beki wakati wa mchezo huo...
Salum Telela, yeye siku hiyo alikuwa na vya 'kidhungu' zaidi...
Malimi Busungu, akiwakalisha mabeki wa SC Villa....
Kaseke akienda kumchungulia kipa na kuchezewa rafu kwa kudakwa miguu na kipa huyo na kusababisha penati....
Akidakwa mguu na kupatikana penati iliyopigwa na Simon Msuva na kupaa juu ya lango.
Kikosi cha Yanga....
Kikosi cha SC Villa...














No comments:
Post a Comment