Na Mwandishi Wetu, Dar
MWANAHABARI
Michael Shija Machellah aliyewahi kufanya kazi katika Kampuniya New Habari 2006 Ltd, inayozalisha Magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba na baadaye
Business Times na Majira amejitosa kwenye mbio za kuwania Udiwani Kata ya Makumbusho jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumzi uamuzi wake huo, Machellah, alisema ameamua kutia nia ya kuwania kiti hicho baada ya kujitafakari kwa
kina mwenyewe kutoka moyoni akiwa na nia thabiti ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika eneo analoishi endapo
Chama CHA CCM kitampa ridhaa ya kugombea eneo hilo na kuking’oa Chama cha CUF, kinachoshikilia kiti hicho.
Alisema
Machellah yeye nimzaliwa wa Mwananyamala, Kata ya Makumbusho na anaishi Kata
hiyo jijini Dar es Salaam
hivyo ana kila sababu ya uzalendo wa kutia nia kwa maana halisi ya kutaka mabadiliko katika
Kata yake kupitia CCM.
Machellah
alizaliwatarehe 19/08/1975 Katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Saalam, alipata elimu ya Msingi Kijijini kwa Wazazi wake Mwime Kahama Mkoani Shinyanga,
Alipata Elimu ya Secondari katika Seminari ya Mt.Joseph Ujiji Mkoani Kigoma na ana Diploma
ya taaluma ya Uandishi wa Habari ambayo aliipata jijini Dar es Salaam katika Chuo cha
Dar es Salaam School of Journalism (DSJ).
Machellah
kwa sasa ni Mwajiliwa katika Kampuniya Integrated Communications Limited
kama Afisa habari katika kitengo cha Mawasiliano na mahusiano (PR) cha moja ya vitengo vya Kampunihiyo.
Wito kwa wakazi wa
Kata
ya Makumbusho kwa mwaka huu wa uchaguzi wasifanye makosa waliyolifanya awamu iliyopita jiandae vyema kukirudisha
Chama cha Mapinduzi Madarakani katika Kata yako na zaidi Mchague Michael
Machellah (NGOSHA) kwa maendeleo ya Kata yako ya Makumbusho.
No comments:
Post a Comment