Habari za Punde

*MWANZA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMDHAMINI BERNARD MEMBE

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Juni 21.2015, wakati akitafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 2,300 walimdhamini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mwenye miwani), akiupungia mikono umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliofurika nje ya viwanja vya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Juni 21.2015, wakati akitafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 2,300 walimdhamini. Picha zote na John Badi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.