Habari za Punde

*NJOMBE WANUFAIKA NA ZIARA YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

Mkurugenzi wa Wilaya ya Njombe,Paulo S. Makala, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Illuminatha Mwenda, Mara baada ya kumaliza mbio zake ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako, mwishoni mwa wiki iliyopita.
******************************************
Halmashauri ya Mji w Njombe wanayo furaha kubwa  kuupokea, Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza, kwa mwaka huu wa 2015.

Ukiwa katika ziara yake Njombe Mwenge wa Uhuru, uliweza kuzindua jumla ya miradi 9 yenye thamani ya Shilingi 2,796,043,527.00 ikiwemo miradi 2 yenye thamani ya Shilingi 80,915,850.00 na kukagua miradi 2 yenye thamani ya Shilingi 2,019,861,000.00, iliyowekewa mawe ya Msingi.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa NSF Juma Khatibu Chum (kulia) akizindua Maabara ya Kemia ya Shule ya Sekondari Yakobi wakatia wa Ziara ya Mbio za Mwenge katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo
*****************************
Miradi mingine yenye thamani ya Shilingi 195,701,282.00 imewekewa mawe ya ufunguzi, na miradi 2 yenye thamani ya Shilingi 470,265,395.00 ilizunduliwa.
Bw. Khatibu, akitembelea kukagua maabara hiyo baada ya kuzindua rasmi.
*******************************
Aidha mikopo yenye jumla ya Tsh 29,300,000.00 imetolewa kwa vikundi 12 vya wanawake (18,000,000.00) na vikundi 18 vya vijana (11,300,000). 

Miradi hii inatekelezwa kwa kushirikisha Wahisani, Serikali, Halmashauri na nguvu za wananchi.

Imetolewa na
Afisa Habari
Halmashauri ya Mji Njombe

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.