Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na
waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma
usiku huu baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu kilichoanza mchana wa
leo, ambapo amesema kuwa Kamati imemaliza kazi yake ya kupitisha jumla ya
majina matano ambayo yatatajwa kesho saa nne asubuhi kabla ya kuingika katika
kikao cha kesho.
Wakati Nape akitangaza taarifa hiyo naye Mjumbe wa Kamati
Kuu, John Nchimbi, alitoka nje ya lango hilo na kutoa tangazo kuwa wanahabari
wasiondoke kwamba wasubiri baada ya dakika ishirini atakuja kuzungumza nao, na
ndipo alipomaliza Nape na Nchimbi aliwakusanya
wanahabi na kusema kuwa Yeye na wenzake watatu, wamegomea matokeo hayo
na kutangaza kujitoa rasmi ujumbe wa Kamati hiyo.
Nchimbi, aliwataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Sophia
Simba, Adam Kimbisa na yeye mwenyewe.
"Kwa hiyo sisi watatu tunatangaza kutoyaunga mkono
matokeo hayo na tanajitenga na matokeo hayo'', alisema Nchimbi.
Nchimbi, akiwatangazia wanahabari kuwataka wasiondoke eneo la tukio na badala yake kuwataka wasubiri baada ya dakika 20 ili arudi kuwatangazia maamuzi ya wajumbe wenzake walioafikia kugomea matokeo.
Wengine walikuwa wakitoka wamenuana na wengine wakiwa wamefurahi, kama anavyoonekana Lukuvi akitabasamu huku akionyesha ishala ya Dole kuwa mambo ni poa.
Wanahabari wakisubiri kupata matokeo usiku huu kabla ya Nape kutoka na kutangaza kuwa majina hayo yatatangazwa kesho majira ya ssa nne asubuhi.
Wanahabari wakisubiri kupata matokeo usiku huu kabla ya Nape kutoka na kutangaza kuwa majina hayo yatatangazwa kesho majira ya ssa nne asubuhi.






No comments:
Post a Comment