Habari za Punde

*DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA WAZIRI CELINA KOMBANI MIKOCHENI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani kilichotoke Nchini India juzi, wakati Makamu wa Rais alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akiifariji familia ya marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifariji watoto wa Familia ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni  

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.