Habari za Punde

*LOWASSA ALIPOHUTUBIA KATIKA ZIARA YAKE YA KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Badiadi kupitia CHADEMA, Godwin Simba, mara baada ya Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015. Katikati yao ni Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye na Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.