Habari za Punde

*MABADILIKO YA KAMATI NDOGO ZA TFF

Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichofanyika Septemba 06, mwaka huu kilifanya mabadiliko madogo ya kamati zake ndogo ndogo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Blassy Kiondo aliyekua Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni na Sakafuni (Beach Soccer and Futsal).
Amina Karuma ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake nchini (TWFA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake.
*COPA COCA COLA KUFANYIKA MWAKANI
Mashindano ya Copa Coca Cola yanayodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Coca Cola yaliyokuwa yafanyike katikati ya mwaka huu, sasa yatafanyika mapema mwakani mwezi Februari kuanzia ngazi ya Wilaya na fainali zake kufanyika mwezi Juni na Julai 2016. KUSOMA ZAIDI BOFYA LINK HIYO CHINI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.