Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwa umezuliwa njiani na wananchi katika eneo la Rudewa, wakati akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro jana, Septemba 25, 2015.
Mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro, akiwa amembeba mtoto wake mabegani huku akimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya wananchi kuzuia msafara wake katika eneo la Rudewa, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro jana.
Msani wa Bongo Movie, Vincent Kigosi maarufu kwa jina la Ray, akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika jana, Septemba 25, 2015, katika jimbo la Kilosa mkoani Morogoro. Ray ambaye awali alikuwa Ukawa, sasa yupo CCM katika kampeni inayoitwa "Nimestuka".
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika jana Septemba 25, 2015, katika jimbo la Kilosa mkoa wa Morogoro..
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Kilosa mkoani Moroogoro. Picha na Bashir Nkoromo





No comments:
Post a Comment