Donald Ngoma wa Yanga (katikati) akichuana na beki wa Mtibwa Sugar..
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia na kumpongeza Donald Ngoma baada ya kuifungia timu yake bao la pili.
Kelvin Yondan akichuana na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia na kumpongeza Donald Ngoma baada ya kuifungia timu yake bao la pili.
Kelvin Yondan akichuana na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.
Beki wa Mtibwa Sugar, Baba Ubaya (kulia) akichuana na beki wa Yanga Juma Abdul.
************************
TIMU za Yanga na Azam Fc, leo zimeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake na kuzidi kuumana kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bar huku Simba nao baada ya kushinda michezo yake mfululizo na kupoteza mmoja dhidi ya watani wao wa Jadi Yanga, leo wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya stand United, bao lililofungwa na Kamwaga katika dakika ya 57 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidhi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kuvunja mwiko wa kupoteza michezo kadhaa katika uwanja huo.
Mabao ya Yaga yalifungwa na Malimi Busungu katika dakika ya 52, akimalizia mpira uliokuwa ukizubaa zubaa baada ya beki wa Mtibwa Suga, Rashid Baba Ubaya kupiga mpira uliombabatiza mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma,wakati akiwa katika harakati za kuokoa na kumchanganya kipa wa Mtibwa na wakati wakivurugana Kipa wa Mtibwa, beki wake na Donald Ngoma, Busungu aliupitia na kuusukumiza wavuni na kuandika baola kwanza.
Bao la pili lilifungwa na Donald Ngoma, katika dakika ya 89, aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa wa Mtibwa, Said aliokuwa akijaribu kupangua shuti lililopigwa na Simon Msuva, aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi kuchukua nafasi ya Salum Telela.
Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Yanga 2- Mtibwa 0.
Nao Azam Fc, pia leo wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam yalifungwa na beki Shomary Kapombe Dakika ya 46 na mshambuliaji Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, Dakika ya 70 yote yakipatikana kipindi cha pili.
MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO
YANGA 2 - MTIBWA SUGAR 0: Jamhuri Morogoro
AZAM FC 2 - COASTAL UNION 0: Azam Complex Dar
SIMBA SC 1 - STAND UNITED 0:- Taifa Dar
MAJIMAJI (1) Zegaga Dk 65 - NDANDA (1) Atupele Dk 50: Songea
AFRICAN SPORTS 0 - MGAMBO JKT 1 Kipanga Dk 1: Mkwakwani
TANZANIA PRISONS 0 - MWADUI 0
KAGERA SUGAR 0 - JKT RUVU 0

No comments:
Post a Comment