Habari za Punde

*TAMISEMI YAENDELEA KUHAMASISHA SUALA LA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli Majuto akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la Feri jijini Dar.Vijana wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika mazingira ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji. 
  Kijana Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
  Kijana Hamisi Misango akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
 Mama lishe Zainabu Hamad anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula katika soko la Feri zoni 4 kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni hapo kwa lengo la kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya wananchi wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
 Baadhi ya maeneo yaliyokithiri kwa uchafu katika soko la Kariakoo.
 Baadhi ya maeneo yaliyokithiri kwa uchafu katika soko la Kariakoo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko la Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha ya uchafu uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda hawachukui tahadhari yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo wanauza matunda aina ya mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi kuyazonga zonga matunda hayo kitu ambacho ni hatari kwa suala la usalama wa afya ya malaji. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.