Mkuu wa Kituo cha
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William
Kisinza akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa
Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao
walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa huo.

Dkt. Robert Malima akitoa maelezo ya namna
watafiti wanavyofanya utafiti na kuwakusanya mbu katika chumba maalum cha
kufanyia utafiti kwa waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari
wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani
walipotembelea Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani
mkoani Tanga mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa
huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Mfanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Masha Mfinanga akichambua viluwiluwi vya
mbu na kuviweka kwenye kifaa maalum tayari kwa hatua nyingine za utafiti.
Sungura waliofugwa
katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga
kwa lengo la kuwalisha mbu wanaofanyiwa utafiti, sungura mmoja ana uwezo wa
kulisha mbu 1500.
Baadhi ya waandishi
wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi
ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani wakimsikiliza Mkuu wa Kituo cha
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William
Kisinza (hayupo pichani) walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea
namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Mkuu wa Kituo cha
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William
Kisinza akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka Kituo cha
Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka
nchini Marekani mara baada ya kutembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea
namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo. Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO,Tanga
************************************************
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO, Tanga.
Tanzania imekuwa nchi
ya kwanza duniani kufanya majaribio ya kupambana na mbu waenezao magonjwa
mbalimbali ikiwemo malaria kwa kutumia kitambaa kilichowekewa viatilifu ili kudhibiti
ugonjwa malaria ambao ni tishio kwa afya ya wananchi wengi wanaoishi vijijini.
Hatua hiyo ya utafiti
imefikiwa na watafiti wa magonjwa ya binadamu katika cha taifa cha Magojwa ya
Binadamu (NIMR) katika kituo cha Amani mkoani Tanga ili kuweza kuwadhibiti mbu
waenezao ugonjwa malaria ambao unaathiri watu wa rika zote nchini.
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga
Dkt. William Kisinza alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha
Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka
nchini Marekani ambao walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna
Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Katika kufanikisha
majaribio hayo, Dkt. Kisinza amesema kituo hicho kinaendelea vizuri na
majaribio ambapo wanatarajia mchanganuo wa utafiti huo utafanyika mwishoni mwa
mwaka 2016 na taarifa kamili itatolewa rasmi mwaka 2017 ili iweze kutumika nchi
nzima na duniani kote.
Dkt. Kisinza amesema
kuwa mafanikio ya taasisi yake yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo na
taasisi nyingine za kitaaluma ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa taasisi
hizo ni Chuo Kikuu cha Afya cha Kilimanjaro (KCMC), Kituo cha Kudhibiti Kuzuia na
Magonjwa cha Marekani (CDC), Taasisi ya Tiba, Dawa na usafi
wa mazingira ya London nchini Uingereza (LSHTM) na Chuo Kikuu cha Brandeis cha
nchini Marekani.
Naye Mtafiti Mkuu anayesimamia
zoezi la majaribio hayo ya mradi huo wa vitambaa vyenye viatilifu hivyo vijulikanavyo
kama “insecticide treated wall liners”, Dkt. Joseph Mugasa amesema kuwa zoezi
hilo linahusisha vijiji 44, kaya zaidi ya 25,000 na idadi ya watu wanaonufaika
na majaribio hayo ni zaidi ya 100,000 katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya
Muheza mkoani Tanga.
Mbali na kuangalia
uwezo wa vitambaa hivyo, mradi huo unaangalia pia uwezo wa vitambaa hivyo
katika kukabiliana na upugufu wa damu kwa watoto chini ya miaka 11, uwezo wa
vitambaa kupambana na mbu sugu kwenye viatilifu vingine na pia kufanya tathmini
ya gharama anazoingia mwananchi katika kugharamikia tiba za malaria.
Kitambaa hicho
ambacho huwekwa kwenye kuta za nyumba kwandani hutumika sambamba na chandarua
ili kuweza kutoa kinga madhubuti mara mbili kumkinga binadamu dhidi ya mbu waenezao
magonjwa.
Mradi huo wa
majaribio wa kutokomeza ugonjwa wa malaria umeanza kufanyiwa utafiti nchini
miaka mtatu iliyopita kuanzia 2013 na unafadhiliwa na Shirika la Misaada la
Marekani (USAID) chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Malaria
(PMI) ambao hadi kukamilika kwake utarajiwa kugharibu zaidi ya Dola za Kimarekani
milioni 3.
Kwa upande wake Meneja
wa Mawasiliano Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkuu
wa msafara wa waandishi hao Dena Gudaitis amesema kuwa wamefurahishwa kuona
Tanzania ilivyosimama imara kujali afya za wananchi wake hasa watu wa kipato
cha chini ambao wengi wao wanaishi vijijini.
Katika kutekeleza
wajibu wao wa kiuandishi, waandishi hao kutoka ICFJ wanaongozwa na kaulimbiu ya
taasisi hiyo inayosema “Andaa mazingira bora ya mwandishi wa habari wa
kimataifa ajaye”.
Waandishi hao wa habari
wamefanya ziara ya siku tano nchini kuanzia Mei 8 hadi 13, 2016 katika mikoa ya
Dar es salaam, Arusha na Tanga ambapo wametembelea baadhi ya zahanati katika
mikoa hiyo, familia zenye watoto walio chini ya mpango wa majaribio wa kudhibiti
malaria, vituo vya utafiti vya Korogwe na Amani pamoja na kiwanda cha
kutengenezea vyandarua cha A to Z cha jijini Arusha.




No comments:
Post a Comment