Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Madeski 50 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pemba Juma kwa ajili ya Skuli ya Msingi ya Mahonda, hafla iliyofanyika kwenye skuli hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pemba Juma akimkabidhi Madeski 50 Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Mhonda Mwalimu Kazima Moh’d Makame
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya Upishi Mwenyekiti wa Kikundi cha Utamaduni cha Akina Mama wa Kijiji cha Kichungwani Bibi Mwema Jumanne ili kuendeleza miradi yao ya kujitegemea.
Balozi Seif akikabidhi fedha kwa Katibu wa CCM Tawi la Zingwe zingwe Nd. Abdulrahman Hassan kwa ajili ya kukamilisha kazi za upigaji plasta wa Tawi lao.
Balozi Seif akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa Tawi la CCM Zingwe zingwe Nd. Omar Juma Omar ajili ya ujenzi wa Mnara wa kuwekea Tangi la Maji safi la Skuli ya Msingi ya Zingwe zingwe.
Balozi Seif akimkabidhi fedha Taslim Imam wa Msiki wa Ijumaa Mahonda kwa ajili ya Shughuli za Tahfidh Quran kwenye kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi Seif akimkabidhi fedha taslim Mwalimu wa Madrasatul Laaila – hailallah ya Kijiji cha Kitope kwa ajili ya kuendeleza harakati za Madrasa hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.
**************************************************
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha wazee kuendelea kuwa mkongojo wa kuwaongoza Vijana wao katika muelekeo wa kukabiliana na matukio ya ajabu yanayofanywa na baadhi ya watu wenye mbinu za kuwapotosha kuelekea kwenye utamaduni na tabia za kijinga.
Alisema wapo watu wasiolitakia mema Taifa hili kutokana na vitendo vyao vya ushawishi wanavyoviekeleza zaidi kwa vijana ili viwatoe kabisa katika misingi ya imani, takwa pamoja na upendo kwa jamii iliyowazunguuka.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi ya Kukabidhi Madeski 50 ya kwanza yenye thamani ya shilingi Milioni 8,500,000/- kati ya Madeski 100 aliyoahidi kwa ajili ya Wanafunzi wa Skuli ya msingi ya Mahonda wakati alipofanya ziara ya kuangalia changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu ndani ya Jimbo lake la Mahonda.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Skuli ya Msingi ya Mahonda na kushuhudiwa na Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma, Naibu wake Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri, walimu, vingozi wa kamati ya skuli pamoja na wanafunzi.
Balozi Seif alisema vijana lazima wajengewe mazingira bora ya kielimu likiwemo suala la kupatiwa vikalio kwani wakati wa wanafunzi kuendelea kuandika kwa kutumia mapaja yao umeshakwisha kabisa.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Jimbo la Mahonda lazima lijengewe miundombinu na mikakati imara itakayotoa nafasi nzuri kwa watoto wake wapate Taaluma itakayotarajiwa hapo baadaye kutoa wataalamu wa fani mbali mbali wakiwemo pia viongozi wa Kitaifa.
Akigusia chuki za kisiasa zinazoenezwa dhidi yake hasa kwa kutumiwa mitandao ya Kijamii ndani na nje ya Nchi Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda alisema tabia hiyo kamwe haitasaidia Wananchi katika kuelekeza nguvu zao kwenye miradi yao ya maendeleo.
Balozi Seif alitanabahisha wazi kwamba wale wanaoacha kufanya kazi zao za kimaisha na kumsema wanaweza kuendelea, na yeye maneno hayo hayatamuathiri lolote kwa vile amekubali kubeba dhima ya kuwatumikia Wananchi kwa nia safi na upendo.
Akizungumza na Wazee, Masheha na Mabalozi wa Jimbo hilo katika Mkutano ul;iofanyika katika Ofisi ya CCM ya Jimbo la Mahonda iliyopo Kinduni Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda alisema wana CCM lazima wawe makini katika kuuepuka mtego wa baadhi ya watu wanaotishia amani ya Taifa.
Balozi Seif alitanabahisha kwamba mbinu na mikakati inayoonekana kutekelezwa na baadhi ya Viongozi wa kisiasa pamoja na wafuasi wao wanaowaamini katika kuchafua utulivu wa kisiasa uliopo baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu inafaa iepukwe.
Mapema Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi aliwahakikishia Walimu, Wanafunzi pamoja na wazee wa Skuli ya Mahonda kwamba vifaa vilivyoahidiwa kutolewa na Mwakilishi wao vitapatikana kwa ukamilifu.
Mama Asha alisema kazi iliyopo kwa sasa ni wananchi kuelekeza nguvu zao katika kujitafutia maisha na kuacha chuki za kisiasa wakati wanafunzi walenge kujitafutia Taaluma itakayowasaidia kuwanasua katika dimbwi la umaskini.
Alisema Wananchi wanapaswa kuwa na tahadhari na watu walioanza uchochezi wa kuvunja moyo viongozi walioamua kujitokeza kwa imani safi ya kuwahudumia Wananchi wao.
Katika ziara hiyo Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Vifaa vya upishi kwa Kikundi cha Utamaduni cha akina mama wa Tawi la CCM Kichungwani pamoja na Fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Mnara wa kuwekea Tangi la huduma za Maji na salama la Skuli ya Msingi ya Zingwe zingwe.
Balozi Seif pia akikabidhi fedha za kumalizia ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi la Zingwe zingwe, Madrasa ya Lailaa – hailallah Kitope pamoja na Jumuiya ya kuhifadhisha Quran Mahonda.
Vifaa vyote ikiwemo Madeski 50 ya Skuli ya Msingi Mahonda,fedha taslimu kutekeleza ahadi aliyoitoa kwa Jumuiya ya kuhifadh Quran, Madrasa na Kikundi cha Utamaduni cha Akina Mama wa Kijiji cha Kichungwani imefikia jula ya shilingi Milioni 14,730,000/-
No comments:
Post a Comment