Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria (aliyekaa katikati) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina ( aliyekaa wa kwanza kushoto) wakiweka saini ya kuiwezesha Serikali kumiliki hisa za TTCL kwa asilimia 100. aliyesimama nyuma katikati kuhuhudia ni Dkt. Maria Sasabo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wengine wa serikali. Hafla hiyo ya kuwekeana saini na iliyofanyika katika ofisi za TTCL Samora jijini Dar es Salaam leo.
Msajili wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru, akionyesha cheti cha makubaliano ya umiliki wa hisa asilimia 35 za Bharti Airtel walizokuwa wakimiliki ndani ya TTCL kwenda serikalini mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel bwana Christian De Faria (kulia) kusainimakubaliano hayo leo.
Picha ya pamoja ni uongozi wa Bharti Airtel na baadhi ya viongozi wa serikali mara baada ya kuwekeana saini ya makubaliano ya umiliki wa hisa asilimia 35 za Bharti Airtel walizokuwa wakimiliki ndani ya TTCL kwenda serikalini.
*****************************************
Tanzania, Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Bharti Airtel Leo wamesaini na kuingia makubaliano ya kuachia hisa zao 35% walizokuwa wakimiliki katika kampuni ya mawasiliano nchini Tanzania TTCL ili serikali iweze kumiliki kampuni hiyo ya TTCL kwa asilimia 100.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria “Bharti Airtel tunaishukuru sana serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri tuliokuwa nao kwa miaka mingi kapitia shirika la Tanzania Telecomunication Company Limited (TTCL).
Bharti Airtel tunatambua mikakati na nia ya serikali kutaka kuwa mmiliki pekee katika shirika la TTCL. kutokana na utaratibu na jitihada zenye maamuzi ya busara toka pande zote Bharti Airtel na Serikali swala hili limefikia tamati.
Hivyo kwa kumalizika vyema kwa swala hili la kuirudishia serikali hisa 35% zilizokuwa zinamilikiwa na Bharti Airtel ndani ya TTCL, Bharti Airtel tunawakikishia watanzania kwa ujumla kuwa tutaendelea na mikakati bora ya uwekezaji kati yetu na serikali kupitia Airtel Tanzania ambapo Bharti Airtel ni mmiliki wa hisa 60%”. alimaliza kusema De Faria
**********************************
About Bharti Airtel
Bharti Airtel Limited is a leading global telecommunications company with operations in 20 countries across Asia and Africa. Headquartered in New Delhi, India, the company ranks amongst the top 3 mobile service providers globally in terms of subscribers. In India, the company's product offerings include 2G, 3G and 4G wireless services, mobile commerce, fixed line services, high speed DSL broadband, IPTV, DTH, enterprise services including national & international long distance services to carriers. In the rest of the geographies, it offers 2G, 3G and 4G wireless services and mobile commerce. Bharti Airtel had over 361 million customers across its operations at the end of May 2016. To know more please visit, www.airtel.com
Regards
email | mailto:Jackson.mmbando@tz.airtel.com
Direct | +255 786 670 120
No comments:
Post a Comment