Beki wa Yanga Juma Abdul, akiwa chini hoi baada ya kupigwa kikumbo na beki wa TP Mazembe, Adama Traore katika dakika ya 28 hadi nje ya uwanja wakati wa mchezo wao Kombe la Shirikisho uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo TP Mazembe waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Kwa ushindi huo sasa TP Mazembe wanaongoza Kundi A wakiwa na jumla ya Pointi 6 na mabao manne ya kufunga huku wakiwa wamefungwa bao moja pekee katika michezo yao miwili baada ya mchezo wao wa kwanza wa nyumbani kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. Katika kundi hilo Mo Bajaia wanashika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 3 na bao moja.
Mabeki wa TP Mazembe wakimdhibiti Donald Ngoma wakati wa mchezo huo.
Juma Mahadhi akimtoka beki wa TP Mazembe wakati wa mchezo huo.
Dk 37 Issama Mpeko alipewa kadi ya njano baada ya kumuangusha Obrey Chirwa, Dk.68 Mbuyu Twite alipewa kadi ya njano
Dk 70 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Mahadhi aliyumia na kumuingiza, Geofrey Mwashiuya.
Dk 71 Yanga tena walifanya mabadiliko kwa kumtoa Obrey Chirwa na nafasi yake akaingia Matheo Anthony, Dk 75 Beki Kelvin Yondani alipewa kadi ya njano baada ya kumcheze rafu Thomas Ulimwengu.
Juma Mahadhi akitoa pande
Deus Kaseke akipiga krosi....
Mashabiki wa Yanga wakiwa na bango linalowakebehi watani zao mashabiki wa Simba
Katika mchezo huo Askari waliimarisha ulinzi kwa kufanya kama askari wa nje wanaokuwa wakiwaangalia mashabiki wakati mchezo ukiendelea badala ya kuangalia mpira.
Benchi la TP Mazembe..
Wachezaji wa akiba wa Yanga
Deus Kaseke akijaribu kuwatoka mabeki wa TP Mazembe
Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya TP Mazembe kupata bao
Wachezaji wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakishangilia....
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha TP Mazembe
No comments:
Post a Comment