Askari Polisi kakikatiza na usafiri wake wa Pikipiki kwenye Barabara ya mabasi ya mwendo kasi na tena akielekea njia isiyoruhusiwa 'No Entry' eneo la Posta ya zamani leo mchana wakati akijua ni kosa kwa watumiaji wa vymbo vya moto na hata maguta kutumia njia hizo. Pamoja na matangazo yote yaliyokwishatolewa lakini bado tu, au ndo kusema waendesha pikipiki au bodaboda wote akili zao sawa??? au ndo kusema 'eti'mtunga sheria ndiyo mvunja sheria???
Mwingine huyu akipishana na basi leney njia yake akigongwa au akikamatwa na kuchukuliwa hatua au kutozwa faini alalamika huyu????
Hapa napo kuna bango linalosomeka hairuhusiwi kukatisha eneo hili la Reli, lakini ndiyo kwaaanza, imekuwa ndo njia ya waenda kwa miguu na wanakatiza tu kama hawalioni bango hili (kulia).
Hawa nao pamoja na kutangaziwa kuondoka lakini ndiyo kwanza mama zao wanazidi kuwabebesha na watoto ili wafanye kazi hii ya kuomba omba katika magari yanayokuwa kwenye foleni, hivi Makonda ataweza kuwaondoa kweli kama alivyotangaza??????
Huyu naye wala hajui kama kuna utaratibu wa kukamatwa na kutozwa faini kwa kutupa taka hvyo, eti kanywa soda yake chupa katembea nayo akiwa kaishika hivi inavyoonekana dirishani kwa dereva, mara kaitupa tu katika bustani ya katikati mwa barabara eneo la Msimbazi Centre.
Hapa kasimama kama anavusha watoto wa shule ndipo akaitupa kabisa kama unavyoona mkono ukimalizia zoezi hilo la kutupa Chupa hiyo iliyozungushiwa duara jeusi. Je huyu akikamatwa na kutozwa faini ya 50, 000 atalalamika au kujilaumu kweli???
No comments:
Post a Comment