MCHEZO wa pili wa washiriki pekee wa Kombe la shirikisho Tanzania Yanga Sc na Tp Mazembe, utakaopigwa siku ya jumanne, kiingilio ni bure.
Hatua hiyo imrkuja baada ya Yanga kutangaza kuwa imefuta viingilio katika mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC na sasa mashabiki wataingia bure.
Akitoa taarifa hiyo jioni ya leo msemaji wa Yanga, Jerry Muro. amesema kuwa lengo la kufuta hivyo ni kuvutia mashabiki wengi zaidi uwanjani wajitokeze kuishangilia timu ya nyumbani dhidi ya timu kutoka DRC.
Awali, Yanga ilitaja viingilio viwili tu katika mchezo huo ambavyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP na tiketi ilikuwa zianze kuuzwa kesho.
No comments:
Post a Comment