Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa nne kushoto) akipokea msaada wa mageti27kutoka kwa Kamapuni ya ving’amuzi ya TINGyenye thamani ya Sh. Million 44 kwa ajili ya kuweka vizuizi kulinda uharibifu wa miundombimu uwanjani hapo katikati ni Mkurugenzi wa kampuni hiyoDkt Vernon Fernandes wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge na kulia ni Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa BwJulius Mgaya.
*******************************************************
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Jumla ya mageti 26 yanatarajiwa kuanza kuwekwa kesho katika maeneo mabalimbali ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzuia uhalifu na udokozi wa miundombinu iliyopo ndani ya uwanja huo.
Akizungumzia kuhusu mpango huo mara baada ya kukabidhi Msaada wa mageti hayo kwa Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura Mkurugenzi wa Kampuni ya ving’amuzi ya TING, Dkt. Vernon Fernandes amesema kuwa ujenzi huo wa mageti katika milango ya maeneo ya uwanja huo utaanza mara moja Jumatatu.
“Vifaa na mafundi wameshafika eneo la kazi na wapo katika maandalizi ya kuanza kuweka mageti hayo na kwa kila siku watakuwa wanaweka mageti saba” alisisitiza Dkt. Fernandes.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ameushukuru uongozi wa TING kwa msaada huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampouni hiyo katika kuboresha na kuendeleza sekta ya michezo nchini.
“Naomba makampuni mengine nchini yaige mfano wa TING ili tuboreshe na kuendeleza michezo” alisema Mhe. Wambura.
Aidha, Mhe. Wambura amewataka wapenzi na watumiaji wa Uwanja wa Taifa kwa shughuli za kimichezo kuwa walinzi wa rasilimali za Umma kwa manufaa ya sasa na ya vizazi vijavyo.
Msaada huo wa mageti 26 kutoka katika kampuni hiyo umekuja mara baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutembele huo mapema mwaka huu na kujionea uharibifu wa miundombinu ambapo kampuni hiyo iliahidi kutoa mageti 26 kati ya 42 yanayohitajika.
No comments:
Post a Comment