Baadhi ya Mashabiki wa Soka wakiwa geti Kuu la kuingilia nje ya Uwanja wa Taifa, baada ya geti hilo kufungwa kutokana na mashabiki kujaa ndani ya uwanja kuzidi uwezo wa uwanja huo. Imeelezwa kuwa mashabiki walianza kuingia ndani ya uwanja huo kuanzia saa moja asubuhi, lakini dosari ikiwa ni wauanja huo kujaa watoto wadogo zaidi waliojihimu kufika asubuhi kuliko mashabiki wa kweli wanaotakiwa kuingia kwa kazi ya kushangilia kwa nguvu zote mwanzo mwisho.
Mashabiki wa soka wakitawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kutangaziwa kuondoka lakini wakawa wakaidi baada ya uwanja kujaa.
Gari la maji likimwaga maji ya kuwasha kuwatawanya mashabiki.
Askari Polisi akikoki silaha yake ili kufyatua bomu la machozi.....
Askari akifyatua Bomu la machozi....
Mmoja kati ya mashabiki akihudumiwa na mwezake baada ya kupiga kirungu na Askari wakati wa zoezi hilo la kutawanya. Shabiki huyo amepasuka kwenye paji la uso
Shabiki huyo akiugulia maumivu baada ya kipigo hicho.
Mashabiki nje ya geti baada ya kufungwa.
Askari wakiwatawanya mashabiki......
Baadhi ya mashabiki wakikimbia kuwahi kuingia uwanjani....kabla ya kuanza kutawanywa....
Mmoja kati ya mashabiki (kushoto) akiruka kutoka ndani ya wanja baada ya kutimuliwa na askari akiwa ndani ya uzio wa uwanja
Mashabiki wakikimbia wakati wakitawanywa
Mashabiki wakitimua mbio baada ya kutawanywa kwa mabomu ya machozi...
Askari wakilinda mabegi ya mashabiki waliosachiwa na kuingia uwanjani ambapo waliamuliwa kuacha mabegi hayo na wakitakiwa kuyachukua baada ya kutoka uwanjani.
Baadhi ya mashabiki wakilalamika baada ya kuanza kwa zoezi la kuwatawanya kwa mabomu.
Baadhi ya mashabiki walikuwa wakinawa maji ili kuondoa uwasho wa mabomu ya machozi.
Kamanda Siro akizungumza na mashabiki kuwatuliza ili wasiendelee kufanya virugu wakati wakitawanywa.
Kamanda Siro, akiwatuliza mashabiki.
Kamanda Siro akizungumza na mashabiki kuwatuliza ili wasiendelee kufanya virugu wakati wakitawanywa.
Kamanda Siro, akiwatuliza mashabiki.
Askari akikimbia huku akikoki silaha yake
Askari akifyatua bomu la machozi
No comments:
Post a Comment