Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amehaidi
kuufanyia kazi mchakato wa kura ya maoni kuelekea upatikanaji wa katiba mpya na
kuendelea nao hapo ulipofikia kwani ni kwa faida ya watanzania wote.
Rais
Magufuli ameyesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhiwa Taarifa
ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji
Mstaafu Damian Lubuva.
Aidha
amesema kuwa kazi imefanyika kubwa na Serikali ya awamu ya nne na mchakato
umefikia sehemu nzuri,hivyo Serikali ya awamu ya Tano wataendelea hapo
ulipofikia pale utakapofikishwa Serikalini kwani lengo ni kuipeleka Tanzania
mahali pazuri.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Mhe.Damian
Lubuva amesema kuwa ucheleweshaji wa kura ya maoni umetokana na muingiliano na
ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na hivyo kushindikana kufanyika.
Pia
amesema kuwa kwa sasa Tume ya Taifa ya uchaguzi itashirikiana na Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar ili kupeleka mapendekezo Serikalini ili kuangalia sehemu
zinazoitaji marekebisho ili yafanyike na kukadhia kuwa hakuna kilichobadilika
zaidi ya muda tu.
Mwenyekiti
huyo ameongeza kuwa Tume imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha Daftari la
wapiga Kura na kwa sasa hawatakuwa wakiandikisha wapiga kura kila baada ya
miaka mitano kwani njia ya Biometric Voters Registration(BVR) kwa mwaka jana
walifanikiwa kuandikisha wapiga kura milioni 23,161,440 sawa na asilimia 96.9
ambapo kanzi data hii itatumika kwa chaguzi zijazo na kurahisisha kuondoa
waliopoteza sifa na waliosajiliwa zaidi ya mara moja na hivyo kufanya daftari
hili kuwa la uhakika na la kuaminika.
Kukamilika kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakamilisha mchakato mzima wa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuashiria kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu
ujao wa mwaka 2020 ambao rais ameagiza uanze mara moja.
No comments:
Post a Comment