Katibu mkuu
wa TAMISEMI, Musa Iyombe akishikana
mkono na Fakri Karim, Meneja Program kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) mara baada ya kusaini makubaliano ya
utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi
Serikali ya
Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), Mfuko wa Umoja
wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) na mashirika mawili yasiyokuwa ya
kiserikali ambayo ni Haki Kazi catalyst (HKC) na Jumuiko la Maliasili Tanzania
(TNRF) wamezindua mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na
tabianchi wazinduliwa.
Mradi huo kwa
mara ya kwanza ulianza kwa majaribio kati ya mwaka 2012 hadi 2013 katika
Halmashauri tatu (3) za wilaya za Longido, Ngorongoro, na Monduli Mkoani
Arusha.
Baada ya
awamu hiyo ya majaribio kumalizika na kuonesha mafanikio makubwa mradi huo umerejea tena awamu hii ukihusisha Halmashauri
nyingine 12 katika mikoa ya Manyara,
Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Lindi na Dodoma na utasimamiwa na TAMISEMI kwa
msaada wa kiufundi na rasilimali fedha kutoka
kwa serikali ya Uingereza
(UK-AID) na Mfuko wa Umoja Wa mataifa wa maendeleo (UNCDF).
Mradi huu
umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2021) ambapo awamu ya
kwanza itaanza kutekelezwa kuanzia mwaka
huu 2016-2018 na awamu ya pili ikianza mwaka 2018-2021.
Kupitia
mradi huo unalenga kuijengea uwezo Ofisi ya Raisi –TAMISEMI katika maene
makubwa mawili ambayo ni uimarishaji wa
taasisi katika uratibu wa mradi na uwezo wa kutafuta rasilimali fedha kwa ajili
ya kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ziweze kutoa elimu kwa jamii kutambua na
kutekeleza Miradi ya kukabiliana na
athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.
Katibu mkuu
wa TAMISEMI, Musa Iyombe
aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Goerge Simbachawene katika uzinduzi huo,
anasema kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi sasa
ni tatizo kubwa na tayari yamelta madhara
makubwa katika maisha ya binadamu
na pia katika uchumi wa taifa na kuleta mzigo mkubwa kwa taifa la Tanzania.
Kunizio
Manyika, Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Lucy Ssendi,
Mkurugenzi Msaidizi, TAMISEMI, akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Alais
Morindat, Mwakilishi Msahuri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), (IIED) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Picha ya Pamoja
No comments:
Post a Comment