Mbunge
wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti
Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa
Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku
mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini
Dodoma.
*******************************************
Na Ismail Ngayonga, MAELEZO - Dodoma
SERIKALI katika mwaka 2016/17 imepanga kujenga nyumba 4139 za askari wa jeshi la Polisi nchini, hatua itakayosaidia kukabiliana na uchache wa nyumba za kuishi kwa askari hao.
Awamu ya kwanza ya nyumba hizo zinatarajiwa kujengwa katika mikoa 17 nchini ikihusisha mikoa ya Tanzania Bara pamoja na mikoa ya Unguja na Pemba.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Faida Mohammed Bakar, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema Serikali itaendelea kuboresha makazi ya askari na ofisi za polisi kwa awamu kwa kadri hali ya kiuchumi itavyoimarika.
Ole Nasha alisema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili askari polisi katika maeneo mbaliombali nchini ikiwemo uchakavu wa ofisi, ambapo kwa kuanzia imeamua kuanza mpango wa kukarabati ofisi na makazi ya askari wake.
Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baadya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
***************************************************************
Aidha alisema Serikali pia imekusudia kuhakikisha kuwa inatoa mikopo ya vyombo vya usafiri kwa askari wake ambao wanaishi mbali na vituo vyao vya kazi ili kuwasaidia kuwahi katika maeneo yao ya kazi kwa wakati.
“Serikali inatambua changamoto inayowakabili askari wetu nchini ikiwemo wale wa Kusini Pemba, katika kukabiliana na hali hiyo tumepanga sasa kuifanyaia ukarabati miundombinu ya ofisi hiyo sambamba na ujenzi wa makazi bora kwa askari wetu” alisema Ole Nasha.
Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kujenga nyumba za kuishi Na ofisi za kisasa katika kituo cha mkoani na kengeja Pemba.
No comments:
Post a Comment