Habari za Punde

*TIMU ZATAKIWA KUWASILISHA MAJINA YA VIWANJA LIGI KUU BARA NA DARAJA LA KWANZA

 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa taarifa kwa barua kwa timu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi daraja la Kwanza ya Star Times kwa msimu wa 2016/17 kwamba kila timu imetakiwa kuwasilisha jina la Uwanja ambao itakaoutumia kama uwanja wa nyumbani kabla ya Juni 20, 2016 
Barua hiyo iliyotumwa kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) ya TFF imeagiza jina la uwanja huo uende sambamba na taarifa za:
- Vipimo vya uwanja
- Iwapo unaweza kutumika kwa mechi za usiku au la
- Idadi ya vyumba vya kubadilishia nguo ‘dressing rooms’
- Uwezo wa uwanja kuingiza mashabiki
- Mmiliki wa uwanja huo
- Aina ya nyasi (asili au bandia)
Tumezielekeza kwamba iwapo timu haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa wa jirani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (3) Ligi Kuu Tanzania Bara toleo la 2016/17.
Tayari TFF, limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako usajili kuanza Juni 15, 2016. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.
Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi Juni 30, mwaka huu.
Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wacheaji. Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
Pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili,
Ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa  kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.