Na Zainab Nyamka,Dar
MABINGWA wa Afrika, timu ya TP Mazembe inatarajiwa kutua Jijini Dar kesho jumapili June 26 tayari kuvaana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Yanga na wakati timu hiyo ikitarajiwa kutua mwishoni mwa wiki inasemekana kuwa ilishatanguliza mashushushu kwa ajili ya kuichunguza Yanga huku ikisemekana kuwa baadhi ya mashushushu hao waliifatilia Yanga toka hatua za awali za mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia.
Baada ya mchezo huo waligawanyika huku wengine wakiendelea kuifuatilia Yanga na mwengine kuja Jijini kusoma mazingira, Mazembe ilifanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wake wa awali dhidi ya Medeama kwa goli 3-1 huku Yanga ikipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ambapo Yanga pia huenda ikarejea kesho ikitokea nchini Uturuki ilipokuwa imeweka kambi baada ya mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia. Akizungumza Jijini Dar es Salaama jana, Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Alfred Lucas alisema kuwa Mazembe imethibitisha kutua nchini kesho na timu hiyo inatarajiwa kutua na msafara wa watu 32 wakiwemo wachezaji na benchi la ufundi huku wakitazamiwa kufikia katika hoteli ya Serena iliyopo katikati ya jiji.
Alfred amesema kuwa maandalizi ya mchezo kati ya miamba hiyo ya soka yanaendelea vizuri na anaweza kusema yamekamilika kwa asilimia mia moja. "Mazembe wamesema kikosi chao kitawasili kesho Juni 26 tayari kwa mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Africa (FA) dhidi ya Yanga", amesema Alfred.
Wakati hilo linaendelea, mashabiki na wapenzi wa Yanga wameendelea kupata imani baada ya mmiliki wa timu hiyo Moise Katumbi, kuhukumiwa kwenda jela miezi 36. Lakini kwa taarifa zisizo rasmi zinasema kuwa Katumbi ni moja ya watu wanaounda msafara wa Mazembe kuja jijini Dar licha ya mahakama nchini DR Congo kutoa hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment