Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongea na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) (hawapo pichani) wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa TUGHE tawi la Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Long’ida Oltetiai akitoa
taarifa ya tawi hilo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi
kwenye ofisi za Wakala hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni
mwa wiki jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala
hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar
es salaam.
Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi kwenye ofisi za Wakala
hiyo ziliopo Mtaa wa Samora, Jengo la Extelecoms mwishoni mwa wiki jijini Dar
es salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) mara baada ya uzinduzi wa
baraza hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
************************************************
Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO
Watumishi
wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) wameaswa kuweka vipaumbele na mikakati ya
kusimamia mifumo ya TEHAMA inayoboresha utendaji kazi na kutoa huduma ili kuongeza
kasi ya ukusanyaji wa mapato ndani ya Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki wakati akizindua baraza la wafanyakazi la
Wakala hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
“Nataka mbuni na kutengeneza mifumo tumizi
mipya pamoja na kuiboresha mifumo tumizi iliyopo ili kuongeza tija kwenye sekta
za kimkakati hususan sekta za afya, kilimo, utalii, elimu, viwanda na biashara”
alisema Kairuki.
Waziri
Kairuki aliyataja maeneo mengine ambayo yanapaswa kuboreshwa katika ukusanyaji na
kutiliwa mkazo katika ukusanyaji wa mapato kuwa ni pamoja na sekta za fedha,
rasilimaliwatu, ardhi na utambulisho wa taifa.
Hatua
hiyo ya eGA ya kuboresha mifumo ya TEHAMA itasaidia Serikali kuimarisha uwezo
wake wa kuwa na taarifa juu ya mifumo yake na kukidhi mapato yake na amewataka
watumishi hao wazidishe kasi ya utendaji kazi ili kuendana na kauli mbiu ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu”.
Aidha,
watumishi hao wamesisitizwa kuwa kuundwa kwa baraza hilo la wafanyakazi ni moja
ya nyenzo ya kuishauri Serikali katika ngazi ya taasisi katika usimamizi wa
kazi na rasilimali, utekelezaji wa majukumu, kulinda haki na wajibu waajiri na
wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi na maslahi na
kusimamia haki na usatawi katika sehemu za kazi.
Akizungumzia
utendaji kazi wa Wakala hiyo, Waziri Kairuki amesema kuwa hatakubali kuona
Wakala hiyo kuwa ni sehemu ya tatizo kwenye utendaji kazi wa kila siku bali watumishi
wafanye kazi kwa weledi na kuwa na mchango katika kuzipatia suluhisho
changamoto zinazoikabili Serikali kwa sasa.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri
Bakari alipokuwa akimkaribisha Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma
alisema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa
eneo la ofisi ambapo hadi sasa wanatumia gharama kubwa katika kukodisha jengo
ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Dkt
Bakari alitaja changamoto nyingine kuwa ni ongezeko la tishio la usalama
mtandaoni kutokana na ukweli kuwa kadiri Serikali inavyozidi kuhamia mtandaoni,
hali ya uhalifu nayo inahamia mtandaoni.
Katika
kutimiza majukumu yake, hadi sasa Wakala ya Serkali Mtandao ina wafanyakazi wapatao
94 ambapo inatarajiwa kuwa jumla ya watumishi 126 mara Serikali itakapotoa
kibali cha kuajiri watumishi wapya.
Wakala
hiyo imejenga historia mpya ya kuwa na viongozi wa kwanza wa baraza hilo ambapo
Donald Samwel amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza kwa kura 29 zilizopigwa za
wajumbe wakati Dianah Mlokozi naye ameingia kwenye historia hiyo kwa kuchaguliwa
kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Baraza
la wafanyakazi la eGA limezinduliwa kwa mujibu wa kutekeleza Sera ya
kuwakilisha wafanyakazi mahala pa kazi kkama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya
majadiliano katika utumishi wa Umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini Na.
6 ya mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment