Mjumbe
wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya
kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma.
Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media
Car Wash Grace Nacksso.
Msanii wa Bongo Fleva Inspekta Harun akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Wajumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija, Maelezo
*********************************************
Na: Frank Shija, MAELEZO
Zaidi ya waandishi wa Habari 1000
kutoka vyombo mbalimbali kunufaika na Mfuko wa Bima ya Afya kupitia msaada
kutoka kwa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es
Salaam na mjumbe wa kamati hiyo Peter
Nyanje wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambe ya maalum ya
kuosha magari Media Car Wash for health itakayofanyika tarehe 25 Juni mjini
Dodoma.
“Lengo la harambee hiyo ni kukusanya
zaidi ya fedha takribani shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima
ya Afya waandishi zaidi ya 1000 hapa nchini.”Alisema Nyanje.
Nyanje amesema kuwa harambe hiyo
itakuwa ni yapili ikitanguliwa na ile iliyofanyika katika viwanja vya Leaders
jijni Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo
zilisaidai kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa taabani.
Aliongeza kuwa na harambee hiyo imekusudia kuhakikisha
waandishi wengi zaidi wanakatiwa Bima ya Afya, ili kujikinga na kadhia ya
kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi.
Kwa upande wake Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso ametoa rai
kwa Wabunge, viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma kujitokeza kwa
wingi katika katika viwanja vya Jamhuri ili kushiriki katika zoezi hilo ambapo
watu wataoshewa magari yao na watu maarufu wakiwemo wasanii wa Bongo fleva ,Bongo
Movie na Miss Tanzania Lilian Kamazima.
Grace amesema kuwa wao kama waratibu wa
harambee hiyo wamejidhatiti kuhakikisha harambee hiyo inafanyikiwa ili kutimiza
azma ya kusaidiana miongoni mwa wanataaluma ya habari nchini.
Harambe ya Media Car Wash
itakayofanyika mjini Dodoma inatahudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wasanii
Joh Makini, Inspekta Haroun, Nikki Wa Pili, G. Nako, Aunt Ezekiel,Kajala
Masanja, Ray Kigosi, Jacob Steven (JB) pamoja na Miss Tanzania Lilian Kamazima
No comments:
Post a Comment