Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi Nasama
Massinda akiwasilisha mada leo Mjini Dodoma kwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Biashara, Viwanda na
Mazingira na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji ( hawapo pichani) kuhusu uanzishwaji wa
Masoko ya Bidhaa hapa nchini ili kuwainua wakulima.
Mkurugenzi
wa Usimamizi na Uendelezaji wa Masoko Kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana Bw. Godfrey Malekano akijibu hoja za Wabunge (hawapo pichani) kuhusu
hatua zinazochukuliwa katika kuwasaidia wakulima kupitia Masoko ya Bidhaa ili
waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha.
Mbunge wa Newala Mjini Mhe. George Mkuchika akichangia mada juu ya namna bora ya kuwainua wakulima hapa nchini hasa wanaozalisha Korosho na mazao mengine ya biashara wakati wa semina kuhusu Masoko ya Mitaji na Dhamana iliyofanyika Mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia mada kuhusu Masoko ya Bidhaa iliyowasilishwa wakati wa
Semina ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Biashara Viwanda na Mazingira
na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo kuwainua
wakulima hapa nchini.
*********************************
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Kilimo kinachangia asilimia 26 ya pato la Taifa na kuchangia zaidi ya asilimia 75 ya kipato kwa wananchi waishio vijijijini, pamoja na mchango mkubwa wa kilimo kwenye uchumi wa nchi, wakulima wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali ya masoko yenye bei zenye ushindani.
Kwa kuliona hilo Serikali ilipitisha sera ya masoko ya bidhaa mwaka 2014 kwa kuanza na mazao manne ya majaribio ambayo ni, Korosho, Ufuta, Alizeti na Mchele.
Hayo yamesemwa leo, mjini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi. Nasama Massinda wakati wa semina kwa Wabunge juu ya uanzishwaji wa masoko ya bidhaa nchini iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.
Akieleza kazi kuu za soko la bidhaa Massinda amesema kuwa soko la bidhaa linaleta uwazi wa bei za mazao na mwenendo wa soko, kila mtu ataweza kujua bei ya mazao sokoni ambapo bei zitatolewa kwa vyombo vya habari pamoja na kuondoa ulazima wa wakulima kusafirisha mazao yao toka eneo moja kwenda lingine kutafuta wanunuzi.
“Vile vile soko la bidhaa litasaidia kutoa bei zenye ushindani kwa kuzingatia upatikanaji wa bidhaa na mahitaji ya bidhaa, litaboresha bei ya mazao vijijini kwa kuwa na soko la bidhaa litakalo toa taarifa kwa wakulima wote kuhusu soko, bei na mwenendo wa soko,” alifafanua Massinda.
Kwa upande wake Mbunge wa Nanyamba, Mhe. Abdallah Chikota alilitaka soko hilo kupanua wigo wa uelimishaji kwa kushuka mpaka kwa wakulima na watendaji wa Serikali katika ngazi ya chini kuliko kuishia kwa mawakala ambao wanaweza wasitoe elimu hiyo kama ilivyotarajiwa.
Soko hilo la Bidhaa linalotarajia kuanza Septemba mwaka huu linategemea kumnufaisha mkulima mdogo, wakulima wakubwa, wenye viwanda, wakusanya mazao (ushirika), wauzaji mazao nje, wakopeshaji na vyombo vya fedha pamoja na Serikali kupata mapato kupitia tozo kutokana na uwepo wa takwimu na uwazi.
No comments:
Post a Comment