Na Zainab Nyamka, Dar
ZIKIWA zimesalia siku Nne kuelekea mtanane wa kukata na shoka unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga na wa soka kwa ujumla, katia ya Mabingwa wawakilishi pekee wa kimataifa Yanga dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kupigwa Juni 28, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kikosi kinaendelea vizuri na zaidi hali za wachezaji wote na wale waliokuwa majeruhi, wapo kwenye hali nzuri na tayari Oscar Joshua ameshaanza mazoezi na wenzake.
Salehe amesema kuwa wachezaji wameendelea na mazoezi jioni ya leo katika viwanja vya hotel ya Rio katika jiji la Antalya huku wakionekana kuwa na morali ya hali juu na wamejiandaa kufanya vizuri katika mchezo wao huo na zaidi watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani.
“wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hata Oscar ameshaanza mazoezi na wenzake na zaidi wameonyesha morali ya hali ya juu kuelekea mchezo huo na wamelihakikishia benchi la ufundi kuwa watatoka na ushindi hasa baada ya makosa yaliyojitokeza na kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Mo Bejaia,”amesema Saleh.
Mbali na hao pia hali ya Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Said Makapu wanaendelea vizuri kwani walikuwa kidogo wanaumwa na watajumuika na wenzao kwa ajili ya mazoezi.
Naye mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa kutokana na uchakavu wa jenereta na kutokuwa kwenye hali nzuri ya kutumika wameamua mechi yao dhidi ya TP Mazembe ipigwe majira ya saa kumi Jioni siku ya Jumanne Juni 28.
“Mechi itachezwa saa kumi jioni hasa baada ya jenereta la uwanja kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi vizuri kutokana na uchakavu wake kwa hiyo mashabiki wa Yanga na wanachama wajitokeze kwa wingi kuja kuishangilia timu yao kwa morali kubwa na kuipa sapoti dakika zote 90, amesema Muro.”
No comments:
Post a Comment