Habari za Punde

*WATAKAOFLASHI SIMU BANDIA KUTOZWA FAINI YA SH. MILIONI 30

 Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu utaratibu wa kuzima simu Feki lililokwisha tangazwa na Mamlaka hiyo kuwa zoezi hilo litafanyika kama lilivyopangwa tofauti na maneno ya baadhi ya watu yanayosikika mitaani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),Mhandisi James Kilava, akiwaeleza waandishi wa habari kuwa zoezi la uzimaji simu  Bandia leo alikwepeki na kutangaza kuwa wale wote watakaojihusisha na vitendo vya kuflash simu watapigwa faini ya shilingi milioni 30.

Aidha Kilava, alisema kuwa licha ya kutaka watu kuacha kutumia simu bandia pia mfumo huo upo kwa jaili ya kuhakikisha usalama wa mtumiaji simu na kwamba mtu yeyote atakaye fanya hivyo atapambana na mkono wa sheria.

"Suala la uzimaji lipo palepale hakuna mtu atakayeweza kuepuka suala hili hivyo nawaomba wale wote wenye simu bandia waanze kuzisalimisha wenyewe mapema.'' alisema Kilava
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini  mkutano huo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.