Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo
wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu
ya watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.
Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae
pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani) wakati akizungumza katika
mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Jimbo ambapo alitoa taarifa juu ya
watu wazima kuanzia umri wa miaka 70 kupata huduma ya matibabu bure.(
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Tawi la Zanzibar, Ismail Kangeta, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya matibabu
itakayoanza kutolewa bure kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa mkutano
uliofanyika Ofisi ya Jimbo.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mwananchi wa Jimbo la Kikwajuni akisoma kilichotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambacho kina majina
ya Hospitali ambazo wafaidika wa huduma ya matibabu bure wanaweza kwenda kupata
huduma hiyo wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo Kikwajuni
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia),
akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kutoa muda wa
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi
wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi ya Jimbo hilo, Zanzibar. Picha
na Mpiga Picha Wetu
No comments:
Post a Comment