*SERIKALI KUANDAA MASHINDANO YA UPANDAJI MITI NA UFUGAJI WA VISIKI HAI
Na Daudi Manongi-Dodoma
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba, amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji wa visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi
cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.
Waziri Makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio
la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi wakati wa Warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Bunge wa
Pius Msekwajijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visikihai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hiyo kuanzia katika ngazi ya chini.
Aidha Mhe. Makamba alisema kuwa upandaji wa miti ndiyo utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani
Nyanja
za Afya, ufugaji, misitu, utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.
Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira. Pia ameahidi Serikali kutenga fedha za kutosha, kutengeneza
Sera nzuri, sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.
Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visikihai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazo husiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visikihai.
Aidha Waziri Makamba amesema kuwa serikali inamkakati mkubwa wa uboreshaji wa
Sera za Mazingira uku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya
Tanzania kuwa ya Kijani.
Warsha hiyo kwa wabunge imeeandaliwa na Shirika
la Lead Foundation kwa kushirikiana na Ofisi ya Bunge na wadau kutoka World Vision,
Ever Green na World Agroforestry Center
ambao walitoa mada mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya kuhifadhi Uoto wa Asili,Kilimo
cha kijani, namna ambavyo ufufuaji wa Visikahai na Ngitili zinavyoweza kuchangia Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na kuimarisha mshikamano kitaifa wa ustawishaji Miti
No comments:
Post a Comment