Wachezaji wa TP Mazembe wakishangilia bao lao lililofungwa Mervrille Bope katika dakika ya 75, katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo TP Mazembe wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga na kujiongezea pointi katika kundi A na kufikisha jumla ya Pointi Sita huku Yanga na Medeama wakiwa hawana Pointi mpaka sasa.
Juma Mahadhi wa Yanga akimhadaa beki wa TP Mazembe.....
Obrey Chirwa akiwania mpira na beki wa TP Mazembe, wakati wa mchezo huo. KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA NA HABARI KAMILI KUHUSU MTANANGE HUO KAA NASI HAPO BAADAYE.
No comments:
Post a Comment