Askofu Dr. Charles Gadi akiongea na
wanahahabari hawapo pichani kuhusu mkutano wa maombi ya kitaifa wa kumwombea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.maombi hayo
yatafanyika geita hivi karibuni
*****************************************
Na
Sheila Simba,Maelezo
Askofu Dkt Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi
kumuunga mkono Rais John Magufuli,katika mchakato wake wa kuamishia serikali makao
Makuu ya nchi Mkoani Dodoma kwani ni uamuzi wa kijasiri na upaswa kuungwa
mkono.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare Es Salaam
Askofu Gadi amesema kuwa jitihada zinazofanywa na Rais magufuli ni kubwa kwani
jitahada zinaonekana wazi za kuimarisha mji wa Dodoma na ili uweze kutumika
kama makao makuu ya nchi.
‘’Serikali inafanya kazi nzuri kinachotakiwa ni
kumtia moyo Rias wetu ili jambo ili lifanikiwe na kuhamisha serikali ili
kutimiza mpango wa muda mrefu wa kuhamisha serikali kutoka Dar es Salaam na
kwenda Dodoma’’alifafanua askofu Gadi
Aidha amesema Serikali imejipanga na inaandaa
mazingira mazuri kwa watumishi wake watakao hamia huko kupata mahitaji yote
muhimu wanayohitaji,na kuongeza kuwa jambo hilo litaharakisha maendeleo katika
mikoa jirani na Dodoma.
Ameongeza kuwa imekua ni kawaida ya baadhi ya watu
kulalamika kila linapotokea jambo bila kusikiliza na kufatilia jambo hilo kwa
makini,amewaomba watanzania wasiwe watu wakulalamika kulaumu na badala yake
wawe watu wakusiliza na kufata maelekezo.
Ameongezea kuwa watafanya maombi ya kumuombea Rais John Magufuli na viongozi wa serikali katika
mji wa buselesele wilaya ya chato mkoani Geita agosti 25 mwaka huu,kuombea
mvua,amani,upendo na mshikamano baina ya serikali na wananchi wake.
‘’Maombi
haya ni ya kumuomba Mungu alifanye taifa letu kuwa taifa bora kwa uchumi,astawi
wa watuwake na linaloongoza kwa amani na mafanikio katika kila sekta
‘’alifafanua Askofu Gadi.
No comments:
Post a Comment