Habari za Punde

*BENKI YA POSTA YAIPIGA TAFU TIMU YA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO (TASWA)

 Afisa Habari na Mawasiliano wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Majuto Omary kwa ajili ya ziara ya mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki tamasha la waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini
 Afisa Habari na Mawasiliano wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi ya sh Milioni 2 kwa Mwenyekiti wa Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Majuto Omary kwa ajili ya ziara ya mkoani Arusha kwa ajili ya kushiriki tamasha la waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Mwenyekiti wa timu ya timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa SC, Majuto Omary akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo.Pembeni ni Afisa Habari na Mawasiliano wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda
**************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeendelea kuisadia timu ya   Waandishi wa habariza michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidh  Sh milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha safari yao ya kwenda mkoani Arusha kushiriki katika tamasha la Waandishi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Afisa Mawasiliano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Chichi Banda alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini.

Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo inakwendakuteteaubingwa wake katika tamashahiloambaloufanyika kila mwaka. Chichi alisema kuwa hii nimara ya tatu kwa TPB kuisaidiatimu hiyo.

Awali TPB ilikabidhi timu hiyo vifaa vya michezo napesa kwa ajili ya ziaraya mkoani Arusha na kufanikiwa kufanya vyema katika ziara hiyo kwa kuutwaa ubingwa ambao ina kwenda kuutetea mwaka huu.

“Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.

Mwenyekiti waTaswa SC, MajutoOmaryaliishukuru TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia pesa hizo kwa ajili ya kufanikisha ziara yao katika maadhimisho ya tamasha la waandishii wa Habari jijini Arusha.

“Tunajivunia uwepo wa Benki ya Posta kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha ziara zake,” alisema Majuto.

Majuto alisema kuwa bado timu yao inahitaji msaada zaidi ili kufanikisha ziara hiyo ambayo itawajumuisha wachezaji wa soka na netiboli. “Tunaishukuru Benki ya Posta, pia tunawaomba wadau wengine nao waunge mkono, muda bado upo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.